MKURUGENZI MKUU WA NEMC DKT. IMMACULATE SWARE SEMESI ATEMBELEA MRADI WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI-KONGWA


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi ametembelea mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa lengo la kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilipofikiwa, ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake na kushauri namna bora ya kuenenda katika ukamilishaji ili kuleta tija na ufanisi kwa maendeleo endelevu ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika ziara yake hiyo, Dkt Sware amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt.Omary A. Nkullo, pamoja na wataalamu wa mazingira kutoka NEMC, TAMISEMI, Halmashauri na Kampuni ya FECE katika kikao cha pamoja cha mrejesho wa ziara ya wataalamu ya ukaguzi wa miradi ya kimazingira inayotekelezwa katika kijiji cha Chimotolo Kata ya Ugogoni Wilaya ya Kongwa na kushauri namna bora ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Kadhalika Dkt. Sware pia amepata fursa ya kuzindua zoezi la upandaji miti eneo la mradi ikiwa ni sehemu ya utelezaji wa malengo kusudiwa yenye mrengo unaotoa chachu ya kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yote ya miradi ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.