MKURUGENZI MKUU NEMC DKT. IMMACULATE SWARE SEMESI ASHIRIKI MKUTANO WA URATIBU WA TATHMINI YA MIRADI YA MAZINGIRA INAYOSIMAMIWA NA UNEP-DODOMA


Shirika la Usimamizi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limeombwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa Serikali ya Tanzania kupata fedha za utekelezaji miradi ya kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa wakati wa Kikao cha Uratibu wa Tathimini ya Miradi ya Mazingira inayosimamiwa na UNEP nchini.

Amesema UNEP imeendelea kuwa mshirika wa maendeleo na Tanzania kupitia kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa, Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini (EBBAR).

Maganga alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika miradi hiyo, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imewasilisha maandiko ya miradi mipya ya vipaumbele inayohitaji fedha zaidi kwa ajili ya kuunga jitihada za kimataifa za mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Tunaishukuru UNEP kwa ushirikiano wa karibu na Tanzania katika jitihada za pamoja za kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha jamii yetu na dunia kwa ujumla inaendelea kubaki salama,” alisema Maganga.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi chache duniani zilizobarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za asili ikiwemo misitu ya asili, mito, maziwa na bahari ambapo maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya manufaa ya wananchi na dunia kwa ujumla na kupitia mikataba na itifaki za uhifadhi na usimamizi wa mazingira.

Alisema kutokana na umuhimu wa rasilimali hizo, Tanzania imeendelea kupiga hatua kubwa katika kusimamia na kutekeleza miradi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na washirika wa maendeleo ili kufikia malengo ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Maganga alisema, Ofisi ya Makamu wa Rais pia imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhuisha Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka