​MAKAMU WA RAIS DKT.PHILIP MPANGO AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA ILALA .


Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Isdori Mpango kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani chenye kaulimbiu isemayo "Urejeshwaji wa ardhi, ustahimilivu wa Hali ya jangwa na ukame" ameongoza wananchi wa Dar es salaam katika zoezi la usafi uliofanyika Soko la Ilala.

Zoezi hilo limehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali, akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) Mhe.Khamis Hamza Khamis, Mkurugenzi wa Baraza la Mazingira Dkt.Immaculate Sware Semesi, wakurugenzi wa Halmashauri zote Tano za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Katika hotuba yake, Mhe.Dkt. Philip Isdori Mpango amesema suala la usafi liwe endelevu ili kunusuru uchafuzi wa mazingira unaoambatana na uchafuzi wa Hali ya hewa na magonjwa ya mlipuko yakiwemo kipindupindu.

Amesema " tarehe 05 ya mwezi wa sita kila mwaka ni wiki ya mazingira, hivyo kama watanzania tumetenga wiki hii nzima kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa Mazingira yetu na kufanya kusafi "

"nimeshuka tu hapa nikapokelewa na harufu mbaya kabisa, Sasa namna hii sio sawa, tumefanya hivi ili kuwajengea wananchi wetu hulka ya kufanya usafi mara Kwa mara na sio kusubiri nyakati maalumu."

Amezitaka mamlaka za Mikoa kuweka utaratibu wa kushindanisha Halmashauri masuala ya usafi ili kuleta msukumo wa kutunza na kuhifadhi Mazingira.

Katika hatua nyingine ametoa siku Saba kwa DAWASA kuhakikisha wanatatua kero ya maji yanayotiririka na kuhatarisha maisha ya wafanyabiashara katika soko hilo la Ilala.

Nae Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kutekeleza Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake ili kutunza Mazingira