DKT JAFO AWATAKA WAWEKEZAJI KUZINGATIA UFANYAJI WA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA


Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Dkt.Seleman Jafo amewataka wawekezaji kote nchini kuzingatia ufanyaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira kabla ya uendelezaji wowote ili kunusuru Mazingira.

Ameitoa kauli hiyo leo alipozuru eneo la mto Zira katika Kata ya Ifumbo, Wilayani Chunya ili kujionea mazingira ya mto unaokabiliwa na changamoto za kimazingira kutokana na uchimbaji wa madini uliofanywa na mwekezaji Kampuni ya "G & I Tech Trading Company Limited".

Amesema Serikali ya Mhe.Samia Suluhu Hassan inasisitiza uwekezaji unaozingatia Sheria ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake ili kunusuru Mazingira.

Ameiagiza NEMC kuhakikisha mwekezaji huyu anafanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na kutekeleza masharti yote atakayowekewa ili kutokuleta uharibifu wa mazingira utakaoathiri kizazi cha sasa na baadae