​BANDA LA NEMC CLINIC YA BIASHARA MWAROBAINI WA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA MAONESHO YA SABASABA


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Banda la clinic ya biashara limeendele kutoa elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za kimazingira zinazowakabili wananchi na kizitafutia ufumbuzi kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamedhihirika leo wakati wananchi wakimiminika katika Banda la NEMC kwenye Clinic ya biashara kutatuliwa kero na changamoto za kimazingira zinazowakabili.

Akizungumza na wananchi katika clinic hiyo Bi.Ritha Said amesema suala la Uhifadhi wa mazingira ni wajibu wa kila mmoja na NEMC kama Taasisi inayoshughulika na mazingira jukumu lake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira pamoja na kuishauri Serikali namna bora ya kuenenda katika kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.