𝐏𝐑𝐎𝐅𝐄𝐒𝐀 𝐒𝐇𝐄𝐌𝐃𝐎𝐄 𝐀𝐏𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐍𝐃𝐀𝐉𝐈 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐌𝐂
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe ampongeza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi kwa utendaji na utekelezaji wa mikakati yenye kuleta tija katika suala zima la Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Nchi.
Prof. Shemdoe amezitoa pongezi hizo alipotemblelea banda la NEMC maonesho ya wakulima ( Nanenane) yenye kaulimbiu isemayo " Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi" na kupatiwa mikakati endelevu yenye kuleta tija katika suala zima la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.
Profesa Shemdoe amesema " NEMC mmepata kiongozi mzuri, ni mtendaji, mtekelezaji na mfuatiliaji wa mambo, hakika mazingira yapo salama chini ya NEMC, hongereni sana"
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15