Kitengo cha Manunuzi
Kitengo hiki kinaongozwa na Meneja.
Malengo
Kutoa utaalamu juu ya usimamizi wa michakato ya manunuzi.
Majukumu
- Kusimamia manunuzi na utoaji wa shughuli zote za Zabuni za Baraza isipokuwa uamuzi na utoaji wa mkataba.
- Kumshauri afisa masuuli katika masuala yote yanayohusu ununuzi na uondoshaji mali.
- Kusaidia na kutekeleza utendakazi na maamuzi ya afisa masuuli na Bodi ya Zabuni.
- Kuratibu au kusimamia manunuzi na shughuli za ununuzi wa Baraza na kupendekeza taratibu za uondoshaji mali.
- Kuandaa nyaraka na matangazo ya fursa za zabuni; na kusimamia michakato ya zabuni.
- Kupitia taarifa za tathmini na majadiliano na kupendekeza utoaji wa tuzo ya mkataba kwa afisa masuuli au bodi ya zabuni.
- Kutunza na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato ya ununuzi na zabuni na usambazaji wa bidhaa, vifaa au mali na kusimamia uondoshaji wa mali chakavu.
- Kufanya uhakiki wa mara kwa mara na kutoa hesabu ya mali na vifaa vya Baraza ili kubaini idadi halisi iliyopo kwenye kumbukumbu.
- Kufuatilia mara kwa mara bidhaa, vifaa au mali za taasisi nunuzi kwa lengo la kubaini matumizi mabaya ya mali na vifaa na kupendekeza hatua stahiki za kuchukuliwa.
- Kuandaa taarifa za mara kwa mara kuhusu bidhaa, vifaa au mali zisizotumika, zisizohitajika, zilizooisha muda wake na zilizoharibika.
- Kusimamia uagizaji wa mahitaji ya taasisi nunuzi na viwango na idadi ya bidhaa, vifaa au mali na kutunza orodha au rejesta ya mikataba ya ununuzi iliyoingiwa.
- Kutunza na kuhuisha kumbukumbu za bidhaa, vifaa au mali za taasisi nunuzi.
- Kuratibu shughuli za ununuzi na uondoshaji mali ndani ya taasisi nunuzi.
- Kutayarisha na kuwasilisha ripoti za manunuzi za mara kwa mara