Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Lengo: Kuratibu uundaji wa mipango yaTaasisi na kusimamia utekelezaji wake.
Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji, na Tathmini kina jukumu muhimu katika taasisi kwa kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kwa ufanisi na malengo yaliyowekwa yanafikiwa (Effectively & Efficiently), Kazi zake kuu ni kama ifuatavyo:
Majukumu
Kuratibu na kusimamia maandalizi na Utekelezaji wa Mipango na Bajeti;
Kuratibu uandaaji na kutoa ripoti za maendeleo ya utekelezaji wa miradi na Mipango ya Taasisi;
Kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango na miradi ya Baraza ili kubaini mafanikio changamoto na namna bora ya kuboresha utendaji;
Kuhudhuria na kufuatilia mikutano ya Tathmini ya Matumizi ya Umma inayoitishwa na Mamlaka za Uidhinishaji mara kwa mara."
Kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati kwa maamuzi ya kimkakati;
Kuratibu masuala ya Bunge kwa kushirikiana na Wizara mama;
Kusimamia uundawaji wa mifumo ya kukusanya na kuhifadhi takwimu muhimu za utekelezaji;
Kushauri juu ya Sera na mwelekeo wa maendeleo ya taasisi kulingana na matokeo ya ufuatiliaji na tathmini;
Kupendekeza njia za kuboresha ufanisi wa miradi na matumizi ya rasilimali.