Kurugenzi ya Huduma za Sheria
Malengo
Kutoa utaalamu na huduma katika masuala ya kisheria
Majukumu
- Kutoa huduma za kisheria
- Kutoa Ufafanuzi wa kisheria kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191
- Kutoa huduma za sekretarieti katika Mikutano ya Bodi
- Kutoa huduma za sekretarieti katika Vikao vya Menejimenti
- Kutoa msaada kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mashauri dhidi ya na kwa niaba ya Baraza.
- Kukusanya taarifa na ushahidi unaotakiwa kuhusiana na kesi.
- Kutoa ufafanuzi wa kisheria kwa umma kuhusu uendeshaji wa Baraza
- Kuandaa Mikataba ya kisheria na makubaliano na kusimamia utekelezaji wa masharti katika Mikataba husika kwa kuhakikisha masilahi ya Baraza yanalindwa.
- Kufanya marejeo na kuanzisha taratibu za kisheria za uendeshaji wa Baraza pamoja na kupendekeza maeneo yanayohitaji kuboreshwa.
- Kuhakikisha uhifadhi salama wa hati za kisheria
- Kupitia ripoti mbalimbali za ukaguzi na kutoa maoni ya kisheria kuhusu masuala yanayohusu madai ya Baraza kwa ajili ya utekelezaji.
- Kuratibu upelelezi wa kesi za jinai za mazingira kwa kushirikiana na vyombo vya uchunguzi vya Serikali
- Kushirikiana na Mamlaka za kisheria juu ya kesi za jinai za mazingira