Kurugenzi ya Tafiti za Mazingira (DERM)

Kurugenzi hii ina jukumu la kufanya tafiti, kuandaa maandiko na kutekeleza miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo  maamuzi sahihi kwenye masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia matokeo ya utafiti, taarifa na takwimu zilizopo.

Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi. Utekelezaji wa majukumu unafanyika chini ya Idara mbili zinazoongozwa na mameneja: 1) Idara ya Uratibu wa Tafiti za Mazingira na  na 2) Idara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Maeneo Maalumu.

Lengo

Kuratibu na kuelekeza utekelezaji wa Agenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira (NERA), Usimamizi wa Mifumo ya Mazingira na masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Majukumu

  • Uratibu wa uandaaji, mapitio na utekelezaji wa Ajenda ya Taifa ya Tafiti za Mazingira (National Environment Reseach Agenda, NERA); 
  • Uratibu wa tafiti za mazingira, tathimini na ufuatiliaji wa mienendo ya mifumo ya ikolojia ikiwa ni pamoja na uandaaji wa taarifa za hali mazingira ya pwani na hali ya matumbawe nchini;
  • Uratibu uandaaji na utekelezaji wa Mkakati shirikishi wa Taifa wa Usimamzi wa Mazingira ya Pwani na Bahari (National Coastal Environmental Management Strategy, NICEMS);
  • Uratibu na usimamizi wa Maeneo Maalumu (Environmental Protected Areas, EPAs) na Maeneo Nyeti (Environmental Sensitive Areas, ESAs);
  • Ukusanyaji wa taarifa na tathmini ya maaneo maalumu yaliyoathirika na kuandaa mpango ya usimamizi wa mazingira ikiwa ni pamoja na mifumo ya ikolojia ya milima;
  • Kutoa mwongozo kuhusu masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na utekelezaji wa miradi chini ya Mifuko ya Ufadhili wa Miradi ya Kuhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni pamoja na kufuatilia upatikanaji wa Ithibati ya mifuko hiyo;
  • Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa Mipango na Miongozo ya Hifadhi ya Mazingira kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa mienendo ya mifumo ya ikolojia kwa kushirikiana na wizara za sekta husika, Halmashauri na wadau wengine;
  • Uratibu wa uandaaji na utekelezaji wa miradi na programu zenye lengo la kutatua changamoto za mazingira ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa chini ya mifuko ya kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi;
  • Ushiriki katika utoaji wa michango ya kitaaluma kwenye masuala ya kisekta yanayohusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi;
  • Ufuatiliaji wa masuala yanayojitokeza katika utekelezaji wa mikataba ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi;
  • Uratibu wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za mazingira;
  • Ushiriki katika kuhamasisha programu za elimu ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi; na
  • Uandaaji wa makongamano, majukwaa, semina za mazingira zenye lengo la kuelimisha jamii juu ya uhifadhi, utunzaji na usimamizi wa mazingira.