Kurugenzi ya Utekelezaji na Uzingatiaji wa Mazingira (DECE)
Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi
Malengo
Kuhamasisha ufuatiliaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira
Majukumu ya Kurugenzi
- Kuandaa miongozo ya kuhamasisha uzingatiaji wa Sheria kwa jamii na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa masharti ya vyeti na vibali vya usimamizi wa Mazingira.
- Kuandaa miongozo kwa lengo la utekelezaji wa Sheria.
- Kujengea uwezo wadau katika masuala ya uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria.
- Kuwezesha, kuratibu na kupendekeza uteuzi wa wakaguzi wa mazingira.
- Kufanya kaguzi na ufuatiliaji wa miradi wa miradi kuhakikisha inatekeleza matakwa ya Sheria ya Mazingira na Kanuni zake.
- Kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni zake pamoja na kutoa maelekezo kwa ukiukwaji wa matakwa ya Sheria na Kanuni zake.
- Kutoa miongozo ya namna bora ya usimamizi na utekeketezaji wa taka hatarishi na taka za kieletroniki.
- Kusimamia na kuendesha maabara ya mazingira ya Baraza.
- Kushughulikia malalamiko ya kimazingira pamoja na majanga yanayotolewa taarifa kwenye Baraza.
- Kupitia na kutoa mapendekezo kwa maombi ya vibali vya utupaji majitaka yaliyochakatwa kwenye mazingira.
- Kuchakata maombi ya vibali vya usimamizi wa taka hatarishi na taka za kieletroniki.
- Kushirikiana na Mamlaka Udhibiti na Mamlaka zingine katika kufanya ukaguzi, ufuatiliaji na uchunguzi katika masuala ya Mazingira.