Kurugenzi ya Tathimini ya Mazingira (DESIA)
Kurugenzi inaongozwa na Mkurugenzi
Lengo
Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu tathmini ya athari kwa Mazingira na jamii kwa miradi mipya na iliyopo ianyotekelezwa.
MAJUKUMU
- Kuratibu mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (TAM) na kutoa mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ya mazingira kwa maamuzi ya utoaji idhini ya utekelezaji wa mradi.
- Kuandaa Miongozo ya kusaidia ufanyaji wa TAM na kuisambaza kwa wadau
- Kuwajengea uwezo mamlaka za serikali za Mitaa na Wizara za Kisekta kuhusu masuala ya TAM
- Kusajili na kusimamia utendaji wa wataalam elekezi wa mazingira
- Kuandaa na kutunza Kanzidata ya miradi iliyosajiliwa na kupata vyeti pamoja na ya wataalam elekezi wa mazingira
- Kuandaa mikutano ya kutoa maoni (Public Hearing) kwa miradi inayogusa maslahi ya jamii
- Kutoa elimu kuhusu masuala ya TAM kwa wadau mbali mbali
- Kufanya mikutano wa wawekezaji ili kujadili changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzitatua