UMUHIMU WA UPANDAJI MITI KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.


Mabadiliko ya tabianchi ni ongezeko la muda mrefu la joto la wastani la Dunia ambalo husababisha kubadilika kwa mfumo mzima wa hali ya hewa, ambao mara nyingi matokeo yake huleta athari hasikatika jamiikama vile ukame, mafuriko, kuongezeka kwa hewa ukaa, kupotea kwa maeneo oevu na kuanguka kwa theluji.

Mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili jamii yetu na Dunia kwa ujumla. Kupungua kwa misitu kwa sababu ya uvunaji misitu usiokuwa endelelevu, ongezeko la shughuli za viwanda Duniani, kupungua kwa theluji,mabadiliko ya utaratibu wa mvua , mafuriko,na ukame miongoni mwa jamii nyingi ulimwenguni umekuwa ukisababisha athari hasi za mabadiliko ya tabianchi.

Ili jamii yetu kujinusuru kutoka kwenye changamoto hizi zinazosabanishwa na mabadilikobadiliko ya tabianchi wataalam wa Mazingira kutoka NEMC wanashauri kuwa njia mojawapo ni kupanda miti Kwa wingi katika jamii zetu ili kuokoa maisha ya viumbe hai wengine pamoja na binadamu.

Pamoja na kuwa na faida zake nyingi kama vile kulinda vyanzo vya maji, kuvuta mvua, kuwa makazi ya viumbe hai mbalimbali, kutoa nishati ya kuni, mkaa na kutoa mbao, miti pia husaidia kunyonya na kuhifadhi hewa ukaa inayozalishwa na binadamu kutokana na shughuli zake mbalimbali.

Madhara yatokanayo na hewa ukaa ni pamoja na kutoboka kwa tabaka la Ozoni na kusababisha miale mikali ya jua kuufikia uso wa dunia hali inayosababisha ongezeko la joto na kukauka kwa mimea, ukame na hata maradhi Kwa viumbe hai wengine pamoja na binadamu, hivyo jamii isipojenga tabia ya kupanda miti itababisha kupotea Kwa viumbe hai wote.

Hata hivyo vyanzo vingi vya maji huanzia kwenye sehemu zenye miti mingi(misitu) juu ya milima ambapo huanza kama chem chem kisha vijito halafu maji hutiririka kama mto. Kazi ya mitini kuzuia yale maji kuzama ardhini (mizizi) na pia majani ya miti huzuia maji maji yasichukuliwe kama mvuke.


Upandajimiti na uhifadhi wa misitu nimoja ya hatua muhimu sanakatika kukabiliana na tatizo la ukame katika nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania, na tayari nchi kupitia Taasisi inayosimamia mazingira imeanza mikakati madhubuti ya kupanda miti nchi nzima kuanzia kwa mashuleni chini ya kampeni isemayo "SOMA NA MTI" ambayo tayari ilishazinduliwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Mazingira Dkt. Seleman Jafo.

Upandaji na uwepo wa misitu katika jamii zetu unachangia asilimia 47 ya akiba ya hewa ukaa ya misitu duniani na hutoa asilimia 60 ya miti ya mbao inayotumiwa viwandani duniani, ambayo inaweza kutumika kuzalisha mazao endelevu ya misitu ili kusaidia mchakato wa kimataifa wa kuingia katika uchumi unaojali mazingira. Kudumisha uwiano kati ya uhifadhi na uzalishaji katika mabadiliko ya tabianchi kunahitaji mfumo wa sera kamilifu na endelevu.