NEMC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI MZURI WA SHERIA YA MAZINGIRA
NEMC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI MZURI WA SHERIA YA MAZINGIRA
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepongezwa kwa kusimamia vyema jukumu la Mazingira kwa Mujbu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alipokuwa akihutubia katika kongamano la Kitaifa la kujenga uelewa juu ya athari za sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada, lililofanyika katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es salaam
Amesema NEMC kama mdau wa Mazingira mwenye dhamana Kisheria, ameitendea haki nafasi yake kwa kuhakikisha elimu ya Mazingira inazungumzwa na kujadiliwa katika mrengo chanya hali inayoleta uzalendo katika kutenda kuliko kusikiliza kunakoleta faida katika Utunzaji na Uhifadhi wa mazingira.
‘Kwa namna ya kipekee kabisa nipende kulipongeza Baraza la Mazingira NEMC, kwa kazi nzuri ya utunzaji wa Mazingira, kwa kusimamia jukumu lake kwa misingi ya Sheria, hasa pale wanapoishauri Serikali namna sahihi ya kuenenda katika kuyatunza Mazingira, huu ndio uzalendo tunaoutaka katika mazingira yetu, Hongereni sana.’Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Ameongeza kuwa NEMC imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha misingi ya Sheria, Kanuni na taratibu za utunzaji na uhifadhi wa mazingira inafuatwa kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15