NEMC YAJIZATITI KULINDA VYANZO VYA MAJI UJENZI WA BARABARA BUSEKELO
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limedhamiria kusimamia na kulinda vyanzo vya maji katika ujenzi wa barabara ya Katumba โLupaso Wilayani Rungwe yenye urefu wa km 35 Mkoa wa Mbeya ili kulinda Mazingira.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi MkuU wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alipoambatana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) pamoja na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) kwenye uzinduzi wa Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Dkt. Gwamaka amesema barabara hiyo inapita kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na mito inayotiririsha maji yake kuelekea Ziwa Nyasa na hivyo ni lazima wahakikishe ujenzi wake hautaathiri vyanzo hivyo ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa binadamu na viumbe wengine.
โMiradi kama hii ya barabara huwa inafanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira ( TAM) na kwa maeneo hasa ya mito tunakuwa makini zaidi kuona hapaathiriki na ujenzi wa barabara. Tutashirikiana na wenzetu wa Bonde la Ziwa Nyasa kulinda vyanzo hivyo, tusipovilinda vitakauka na hata Ziwa letu litakauka na hivyo kusababisha kukosekana kwa maji, kwa hiyo sisi kama wasimamizi wa mazingira tutahakikisha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 inafuatwa,โ amesema Dkt. Gwamaka.
Aidha, ameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwani ni muhimu kwa ajili ya wananchi kusafirisha mazao mbalimbali yanayozalishwa kwenye eneo hilo.
๐๐ฌ๐ข๐ฌ๐ข๐ญ๐ข๐ณ๐ ๐๐ก๐ข๐๐๐๐ก๐ข ๐ง๐ ๐๐ฌ๐ข๐ฆ๐๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ณ๐ข๐ง๐ ๐ข๐ซ๐ ๐ก๐๐ฌ๐ ๐ฎ๐๐ก๐ข๐๐ข๐ญ๐ข ๐ฐ๐ ๐ค๐๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐๐ก๐๐๐ฎ๐ณ๐ข...
Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingir...
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15

