NEMC YAJIPANGA KUTOA ELIMU KWA UMMA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limejipanga kutoa elimu ya Mazingira katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoadhimishwa katika viwanja vya Chinangali Park kuanzia tarehe 16-23, 2025 Jijini Dodoma.
Akizungumza kuhusu Maadhimisho hayo, Kaimu Meneja Kanda ya kati Bw. Novatus Mushi ameeleza kuwalengo la Baraza katika Maadhimisho hayo ni kuonesha huduma mbalimbalizinazotelewa na Baraza, elimu ya Mazingira, kutoa matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo Baraza linazifanya na juhudi ambazo Baraza linazifanya kuhakikisha watanzania wote wanakuwa katika Mazingira salama.
Ameongeza kuwa Baraza limejipanga kuelimisha wadau mbalimbali hususani wananchi wa kawaida ili waweze kuelewa huduma mbalimbali ambazo Baraza linazitoa kwa umma.
Aidha Meneja Mushi anawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la NEMC ili kupata elimu ya Mazingira na huduma mbalimbali ambazo NEMC inazitoa kwa umma katika suala zima la Mazingira
Maadhimisho hayo yanayoadhimishwa na taasisi, Wizara na Tawala mbalimbali mbalimbali yameambatana na maonesho yaliyojikita kutoa elimu,kuhabarisha na kutoa huduma mbalimbali za papo kwa papo.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15