​NEMC YABAINI UKIUKWAJI WA SHERIA YA MAZINGIRA BANDARI YA DAR ES SALAAM


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limebaini ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Usimamizi na Udhibiti wa taka hatarishi ya mwaka 2021 unaotokana na ukataji wa taka hatarishi eneo la Dockyard KOJ bandari na kupelekea kutiririsha mafuta na taka nyingine baharini.

Akiongea katika eneo la hilo la Dockyard KOJ bandari ambako mabomba ya mafuta ya makampuni mbalimbali yanapita Dkt.Thobias Mwesiga, Kaimu Mkurugenzi idara ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira NEMC amesema utiririshaji wa mafuta kuelekea baharini ni kinyume cha Sheria na kinahatarisha uhai wa viumbe wa baharini pamoja na uchafuzi wa Mazingira na kuyataka makampuni yaliyohusika kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kurejesha mazingira katika hali yake.

" Sisi kama Baraza tumefanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam eneo la Dockyard KOJ ambalo ni eneo yanakopita mabomba ya mafuta ya makampuni mbalimbali, tumebaini ukataji wa taka hatarishi kinyume cha matakwa ya Sheria unaopeleka uvujaji mkubwa wa mafuta yanayotiririka kuelekea baharini na kuathiri viumbe hai wa baharini. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Kanuni za Usimamizi na Udhibiti wa Taka hatarishi( Hazardous Waste regulation ya mwaka 2021) . Maelekezo yetu kama Baraza, Makampuni yaliyobainika kufanya makosa hayo kuitwa na kuchukuliwa hatua pamoja na kuhakikisha yanarejesha mazingira katika hali yake