MKURUGENZI MKUU NEMC Dkt. IMMACULATE SWARE SEMESI AZUNGUMZA WAKATI WA UFUNGUZI WA WARSHA YA MABADILIKO YA TABIANCHI DODOMA.


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, azungumza wakati wa ukaribisho wa washiriki katika warsha ya mabadiliko ya tabianchi inayoendelea Jijini Dodoma.

Akizungumza katika warsha hiyo iliyoandaliwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Adoptation Fund) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na washiriki kutoka mataifa 34, amesema ni kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa namna ya kuendeleza miradi hususani ya mabadiliko ya tabianchi na kujengeana uwezo wa namna ya kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi nchini Tanzania.

Amesema warsha hii iliyofanyika katika Hotel ya Best Western Dodoma itakwenda kuwa chachu kwa Taifa katika mapambano dhidi ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa Mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu.