​JAFO AIPONGEZA NEMC MAONESHO YA SITA YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa ustawi wa kizazi cha sasa na cha badae.

Amezitoa pongezi hizo leo alipotembelea banda la (NEMC) Maonesho ya sita (6) ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita kwa lengo la kujiridhisha na elimu ya Mazingira inayotolewa.

"Niwapongeze sana NEMC kwa sababu mmekuwa msaada mkubwa sana katika ofisi yangu hususani katika suala la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira" alisema Waziri Jafo.

Pamoja na hayo, Waziri amelisisitiza Baraza kutumia fursa ya maonesho ya madini kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, madhara ya uharibifu wa mazingira na madhara ya matumizi ya zebaki katija kuchenjulia madini ya dhabu kwa wachimbaji wadogo