​ELIMU YA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA YATOLEWA KWA WADAU-GEITA


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na STAMICO, limetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya zebaki katika Maonesho ya sita (6) ya Kimataifa ya Madini yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Mkoani Geita.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uelewa kwa wachimbaji wadogo kuhusu namna na umuhimu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii, madhara ya afya kutokana na matumizi ya Zebaki, matumizi Sahihi ya Zebaki na njia Mbadala za uchenjuaji bora kutumia Zebaki.

Sambamba na hilo Baraza liliendesha majadiliano na wadau mbalimbali kwa lengo la kuwapa mwanya wa kuweza kutoa maoni na mapendekezo lakini pia kujifunza kutoka katika Taasisi nyingine ili kuweza kuboresha utendaji wa Baraza.