BALOZI WA UMOJA WA ULAYA (EU) NCHINI TANZANIA AKUTANA NA MHE. ZUNGU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KIMAZINGIRA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu afanya mazungumzo na Balozi wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe. Manfredo Fanti kujadili masuala mbalimbali ya kimazingira hasa kwa upande wa mabadiliko ya tabianchi, yaliyofanyika ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mhe. Waziri Zungu ameeleza kuwa lengo la ujio wa ugeni huo ni kuzungumzia masuala mbailimbali ya kimazingira ikiwemo masuala ya mabadiliko ya Tabianchi,Tabaka la Ozoni na maandalizi ya msaada wa bara la Ulaya unaondaliwa kuipatia Tanzania kwa miaka mingine tena kwa ajili ya katika kutuza mazigira. Bajeti yao inaisha mwisho ya mwezi wa kumi na mbili hivyo walitaka tuwaeleze nini kitakuwa kipaumbele kwetu Tanzania kwa miaka miwili ijayo katika maswala ya Mazingira.

Aidha Mhe. Zungu ameeleza kuwaUmoja waUlaya umependekeza tuangazie upande wa nishati mbadala na mpangilio mpya wa miji ulio endelevu katika maeneo yetu, ambao mpango huo utafanikiwakutokana na pesa itakayotoka katika mifuko yao.

“Tumeelewana kuwa tutatoa mapendekezo yetu na wao watasema maeneo ambayo wanafikiri sisi tutahitaji kwa siku za mbeleni kwa mujibu wa mkataba. Pia tumewatahadharisha kuwa kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi, Tanzania pamoja na Nchi zingine za Afrika ndio wahanga wa matumizi mabaya ya viwanda katika nchi za Ulaya. Wamekubali ni kweli nchi zao zinachingia mabadiliko ya tabia nchi kwa kiasi kikubwa hivyo wamesema kuwa wanaongeza pesa katika kudhibiti madhara hayo na kuvibana viwanda vyao kutumia teknolojia mpya ambazo zitapunguza hewa ya ukaa kwenda kuharibu tabaka la ozoni na madhara mengine ya kimazingira, alisema Zungu.

Kwa upande wake Balozi Manfredo Fanti ameeleza kuwa Umoja waUlaya uko tayari kushirikiana na Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi, na maswala mengine ya kimazingira na yote hii ni hatua ya kuleta ushirikiano bora na ulio imara kati ya Tanzani na Bara la Ulaya. Katika kuimarisha uhusiano huo kwa sasa wapo kwenye harakati ya kuandaa bajeti itakayoanza Januari 2021 ambayo itaweza kusaidia maswala mbalimbali ya kimazingira kwa hali ya juu.

Mhe. Zungu Amemalizia kwa kusema kuwa tatizo la uharibifu wa tabaka la ozoni linasababishwa pia na uingizwaji kutoka ulaya wa friji na vifaa vingine vilivyochakaa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya zamani, ambazo sio rafiki kwa tabaka la ozoni. Hivyo amesisitiza kuwe na ushirikiano wa kutosha kati ya Tanzania na Bara la Ulaya katika kupambana na uharibifu wa tabaka la Ozoni, kwani athari zake zinapotokea haziathiriTanzania peke yake bali ni Dunia nzima.