𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐘𝐀𝐑𝐈𝐍𝐃𝐈𝐌𝐀 𝐍𝐙𝐔𝐆𝐔𝐍𝐈 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendelea kutoka elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake katika viwanja vya Nzuguni kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa yanayoendelea Jijini Dodoma.
Banda hilo linatoa elimu ya mazingira ihusuyo: umuhimu wa uzingatiaji ufanyaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, umuhimu wa kutenganisha taka hatarishi kutoka kwenye chanzo, umuhimu wa udhibiti wa kelele zilizozidi viwango, athari za matumizi ya mifuko ya plastiki, umuhimu wa washauri elekezi wa mazingira kujisajili kwa njia ya kielektroniki na umuhimu wa ulipaji wa Ada za Mazingira.
Habari na Matukio
Matukio
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15