𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐖𝐀𝐑𝐄 𝐒𝐄𝐌𝐄𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐓𝐀𝐊𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐁𝐈𝐃𝐈𝐈 𝐍𝐀 𝐖𝐄𝐋𝐄𝐃𝐈


Dkt. Sware Semesi ameyasema hayo Julai 24,2024 alipokuwa anaagana na aliyekuwa Mtumishi wa Baraza Bi. Germana Ijiko ambaye ameazimwa kwenda kuitumikia Wizara ya Fedha.

Aidha Dkt. Semesi ameongeza kwa kusema ni furaha yake kuona watumishi walio chini yake wanaonekana na kuchukuliwa kwenda kuwatumikia wananchi sehemu mbalimbali kwani hiyo inadhihirisha uaminifu uliomo ndani ya watumishi hao lakini pia ni fursa ya kukua zaidi kwenye kazi.