𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐘𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐃𝐀𝐑 𝐄𝐒 𝐒𝐀𝐋𝐀𝐀𝐌 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐅𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki katika zoezi la kufanya usafi wa Mazingira lililofanyika katika Wilaya ya Ilala.
NEMC imeshiriki zoezi hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhamasisha wananchi kusafisha na kutunza Mazingira katika maeneo yao.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa mwenyewe, Mhe. Albert John Chalamila akiambatana Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji, pamoja na watumishi wa Mkoa na Jiji la Dar es Salaam.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesisitizauboreshwaji wa miundombinu ya ukusanyaji na utunzaji taka katika maeneo maalumu ili kutengeneza mbolea na nishati jambo litakaloongeza fursa za ajira pamoja na usafi wa Mazingira ili Jiji la Dar es Salaam liendee kuwa safi na kivutio kwa uwekezaji na utalii.
Washiriki wengine wa zoezi hilo ni pamoja na DAWASA, TANESCO na wafanyabiashara wa maeneo ya Wilaya ya Ilala.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15