𝐓𝐌𝐅, 𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐁𝐎𝐑𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈 𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀
Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) inashirikiana na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuongeza ushiriki wa mameneja wa kanda na watendaji wa kampuni hiyo kwenye kutoa habari kama sehemu ya kuimarisha mkakati madhubuti wa mawasiliano na vyombo vya habari.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi alisema kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuendeleza uelewa wa mazingira kupitia vyombo vya habari. Alisisitiza umuhimu wa kuwapa waandishi wa habari na maafisa wa NEMC ujuzi unaohitajika ili kuwasilisha kwa umma masuala ya mazingira kwa ufanisi.
"Kuimarisha ushirikiano wetu na TMF kutatusaidia kujenga umma wenye uelewa na kushirikishwa zaidi kuhusu masuala ya mazingira, Mafunzo haya ni hatua muhimu ya kufikia lengo hilo." Alisema Dkt. Semesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TMF Bw. Dastan Kamanzi aliwasilisha Mpango Shirikishi wa Kukuza Uandishi wa Habari za Mazingira wa TMF (CEJNP), mpango wa pamoja na Taasisi ya Human Dignity and Environmental Care Foundation (HUDEFO). Mpango huo unalenga kukuza kizazi kipya cha waandishi wa habari wa mazingira ambao wanaweza kutoa hadithi za hali ya juu na zenye athari.
Meneja Mawasiliano wa NEMC, Irene John aliwahimiza washiriki kutekeleza maarifa waliyoyapata kutokana na mafunzo hayo katika kazi zao za kila siku.
"Ushirikiano mzuri wa vyombo vya habari ni muhimu kwa NEMC kutimiza wajibu wake, tunatarajia kuona matokeo yanayoonekana katika wiki zijazo." Alisema Bi. Irene.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15