โWAZIRI JAFO AIPONGEZA BODI YA WAKURUGENZI NEMC KWA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa utekelezaji wa majukumu yake.
Ametoa pongezi wakati akizungumza kwenye kikao cha 16 cha Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya NEMC kilichofanyika leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma.
Dkt. Jafo amesifu utaratibu wa kutembelea maeneo mbalimbali kukagua shughuli za kulinda mazingira hususan katika migodi iliyopo ya mkoani Geita na kwengineko.
โNiwapongeze mwenyekiti na timu yako badala ya kukaa tu ofisini na kuangalia takwimu kwenye makaratasi badala mmekuwa mkienda site hasa migodini na viwandani kuona uhalisia na kulisaidia Baraza mnalosimamia,โ amesema.
Aidha, Waziri Jafo ametoa rai kwa Bodi hiyo kuendelea kuisimamia NEMC inapotekeleza Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika maeneo mbalimbali na kuwachukulia hatua wanaoikiuka.
Amesema kuwa ni jukumu la NEMC kuhakikisha wenye viwanda, migodi na maeneo ya starehe yanafuata sheria ili kudhibiti changamoto za uchafuzi wa mazingira zikiwemo utiririshaji wa majitaka, moshi au kelele na mitetemo.
Hali kadhalika Dkt. Jafo ametoa rai kwa wananchi kufuata sheria na kuepuka vitendo vya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti holela na kuacha kuharibu vyanzo vya maji.
๐๐ฌ๐ข๐ฌ๐ข๐ญ๐ข๐ณ๐ ๐๐ก๐ข๐๐๐๐ก๐ข ๐ง๐ ๐๐ฌ๐ข๐ฆ๐๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ณ๐ข๐ง๐ ๐ข๐ซ๐ ๐ก๐๐ฌ๐ ๐ฎ๐๐ก๐ข๐๐ข๐ญ๐ข ๐ฐ๐ ๐ค๐๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐๐ก๐๐๐ฎ๐ณ๐ข...
Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingir...
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15

