WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA WARSHA YA MAAFISA MAZINGIRA DODOMA


WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA WARSHA YA MAAFISA MAZINGIRA DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amezindua rasmi Warsha ya Maafisa Mazingira iliyojumuisha Maafisa mazingira wa ngazi ya Kitaifa, Mkoa na Wilaya. Warsha hiyo iliyoendeshwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Akifungua warsha hiyo Mhe. Bashungwa amesema " Suala la utunzaji wa mazingira na mikakati endelevu ya utunzaji wa mazingira ni jambo letu sote sambamba na kutoa elimu kwa umma kwa kuzingatia uhitaji wa uchumi wetu." Amewasihi watanzania wote kutunza mazingira kwani ni jukumu la kila mmoja na si la Maafisa mazingira pekee.

Aidha amesisitiza umuhimu wa kutoa mafunzo kwa Maafisa mazingira ili kuwajengea uwezo wa kutoa elimu iliyo sahihi kwa jamii juu ya utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo kusaidia kupunguza athari za mazingira na kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu.