WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU TAKRIBANI 3000 WAFIKIWA NA ELIMU YA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI YA ZEBAKI
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu takribani 3000 Nchi nzima kupitia mradi wa kudhibiti matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo (EHPMP) unaofadhiliwa na Bank ya Dunia wapatiwa elimu ya matumizi salama ya kemikali ya zebaki.
Hayo yamedhihirishwa na Afisa Mazingira Mkuu wa NEMC Bi. Ritha Said alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi katika Banda la NEMC lililopo clinic ya Biashara kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Bi Ritha Said amesema "NEMC tuna dhamana na tunasimamia mradi wa kudhibiti matumizi ya kemikali ya zebaki (mercury) katika shughuli za uchenjuaji, mradi huu unafadhiliwa na benki ya Dunia pamoja na mfuko wa mazingira duniani na unatekelezwa katika mikoa 7 ambayo ina wachimbaji wengi wadogo ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Singida, Mbeya na Songwe."
Ameongeza kuwa mradi huo unaoratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa kishirikiana na Ofisi ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali imetoa elimu ya matumizi salama ya zebaki ikihusisha namna ya kujikinga wakati wa uchenjuaji, umuhimu wa matumizi ya vifaa kinga, athari za zebaki kwa mama wajawazito, umuhimu na faida za kusajili mialo pamoja na athari za kemikali ya Zebaki katika mazingira.
Ameyataja madhara ya zebaki kuwa ni kuharibu mfumo wa fahamu, huleta msongo wa mawazo, kuharibu vinasaba, kuathiri mifumo ya uzazi pamoja na mazingira.
Karibu Banda la NEMC clinic ya biashara upate elimu ya matumizi salama ya zebaki pamoja na elimu ya uhifadhi na usimamizi wa Mazingira
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15