NEMC YAZITAKA TAASISI ZINGINE KUIGA MFANO WA MUHIMBLI KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
NEMC YAZITAKA TAASISI ZINGINE KUIGA MFANO WA MUHIMBLI KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limezitaka Taasisi za Afya za Serikali na binafsi kuiga mfano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa utunzaji wa mazingira.
Hayo yamesemwa leo na Meneja Uzingatiaji wa Sheria na ufuatiliaji NEMC, Bw. Hamad Taimur wakati wa kukabidhi vifaa vya kutenganisha taka, ikiwa ni kilele cha siku ya mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 05, Juni ya kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Pinga uchafuzi wa mazingira utokanao na mifuko ya plastiki’
‘Ukiangalia hapa Muhimbili, mazingira yake ni ya kijani, hakuna taka zinazozagaa na hii imewezekana kutokana na hospitali kuwa na timu inayosimamia usafi wa mazingira ya hospitali, kwakweli hili ni jambo la kuigwa na tunawaasa wengine waje wajifunze hapa’ amefafanua Bw. Taimur.
BwTaimur ameongeza kuwa NEMC inaamini kuwa vifaa vilivyotolewa leo, vitasaidia kuendelela kuboresha shughuli za usafi na utunzaji wa Mazingira wa maeneo mbalimbali ya hospitali kwa kuwa hospitali inazalisha taka za aina mbalimbali ikiwemo taka hatarishi.
Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi wa huduma za ufundi na matengenezo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Domiana John kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji MNH ameishukuru NEMC kwa msaada huo na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuendelea kuimarisha shughuli za usafi hospitalini hapa.
Bi Domiana amesema kipaumbele cha Hospitali ni usafi na usalama wa wadau mbalimbali wanaoingia na kutoka ndio maana imeendelea kuweka mazingira katika hali ya usafi na kuepuka kuzagaa hovyo kwa taka kwa lengo la kuepuka magonjwa mbalimbali.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15