NEMC YATOA WITO KWA NCHI ZA AFRIKA KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI
Serikali kupitiaBarazala Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) na wadau mbalimbaliakiwemo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wameshiriki katika zoezi la upandaji miti takribani 300 lililofanyika katika msitu wa mazingira asili Pugu Kazimzumbwi lililoko Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema mti ni moja ya kiungo cha dunia kinachoiwezesha kuishi kwani inaleta hewa, mvua, chakula na kulinda ardhi.
Dkt. Immaculate Sware amesema “Siku ya leo tunasherekea Mama Dunia na tunamsherekea kwa kupanda miti. Mti ni kiungo cha dunia kinachofanya dunia iishi, kwanimti huo unahakikisha kwamba inachuja hewa, inatuletea mvua, inatupa chakula, inatuletea hewa safi, inatupa biashara na inalinda ardhi. Leo tunamsherekeahuyu mti, tunasherekea hii dunia kama bara la Afrika na Tanzania ikiwa mmoja wapo ya umoja wa Bara la Afrika na hapa tunasuport kubwa ambayo wameianzisha wenzetu kutoka Kenya kwani wao ni wenyeji wa Jumuia ya Mataifa inayoshughulikia Mazingirana tunamsherekea Mama Wangari kwasababu alikwa champion wa Mazingira akitokea Kenya kwa suala la Utunzaji wa Mazingira na alikuwa anasisitiza suala la upandaji miti kwa mtu mmoja mmoja na jamii katika Nchi na Bara letu kwa ujumla na ni mwanamke wa kwanza kwa juhudi zake hizo za kutunza Mazingira alishinda tuzo ya Nobel rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa.”
Naye Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Isaac Njenga alipozungumza amesema “Siku hii ambayo huadhimishwa kila tarere 03 mwezi machi kila mwaka iliahirishwa kutokana na msiba wa Hayati Mzee wetu RaisMstaafu wa awamu ya Pili, Rais Ally Hassan Mwinyi, sasa leo tumekuja hapa katika maadhimisho ya Wangari Maathai Day ambayo pia ni siku ya Mazingira ya Afrika kwa ajili ya utunzi na uhifadhi wa Mazingira na jambo la kutunza Mazingira ni la muhimu . Mama Wangari Maathai Maisha yake yote alitunza Mazingira na hata akawa mwanamke wa kwanza Afrika kupata ile tuzo ya Nobel. Alianzisha vuguvugu lililoitwa green belt movement mwaka 1977 kwa kushirikiana na Ubalozi wa Kenya na tunashukuru sana kwa ujio wa watu wengi ambao ni wakenya waishio Tanzania Pamoja na viongozi mbalimbali wakiweo mabalozi wa Nchi mbalimbali kushiriki nasi, hii imeweka alama kwetu ya kwamba tu wamoja katika suala la Utunzaji na Uhifahi wa Mazingia Afrika.
Balozi Isaac Njenga ameongeza kuwa kila mmoja analo deni na jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba anatunza mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwani mazingira tunayojivuniasasa ni sababu ya kuwapo kwa watanguliziwaliojitolea kwa kupanda miti na kuitunza na leo inasaidia kuzalisha chakula, maji na mahitaji mengine.
Naye Wazir Mstaafu wa Jumuia ya Mataifa anayeshughulikiaMazingira Dkt.Teresa Humisa amesema uchafuzi wa Mazingiraumechangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa Mabadliko ya Tabianchi zinazoambatana na changamoto nyingi za Kimazingira.
Dkt. Teresa amesema “ Mazingira yameharibiwa kwa kiasikikubwa sana, na hata hili joto tunalolipata sasa hivi mtu unasikia unaungua ni kwa sababu ya uchafuzi wa Mazingira, Bara la Aafrika uchafuzi wake umesababishwa na kukata miti kwa ajili ya kupika, mashamba, mbao, kwa hiyo miti imeharibiwa mingi na ndio maana tumefka hapa tulip oleo”
Akihitimisha hafla hiyo iliyoambatana na zoezi la upandaji miti , Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma zaMisitu Tanzania Bi.Carolen Malunde kwa niaba ya Kamishna wa hifadhiwawakala wa huduma za misitu Tanzania amesema msitu huu umepandishwa hadhi kuwa msitu wa mazingira asilia kuanzia mwaka 2020, Msitu huu umebeba histori akubwa ya dunia, unaukubwa wa hekta 8965, una aina 80 za ndege na 14 za wanyama wadogo pamoja na mimea ambayo Iko hatarini kutoweka.
Ameongeza kuwa miti iliyopandwa katika hifadhi hiyo ni ile inayostahimili ukame huku akiitaja baadhi yake kuwa ni migunga na mkangazi ambayo huoteshwa kando ya mto.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15