NEMC YATOA SIKU TISINI (90) UJENZI WA MIUNDOMBINU YA KUTEKETEZEA TAKA HATARISHI KATIKA TAASISI ZINAZOTOA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku tisini (90) kwa Taasisi zote zinazojishughulisha na utoaji wa huduma za afya nchini kujisajili kwenye Wizara husika ili kupata utaratibu mzuri na kupatiwa vibali maalumu vya usimamizi wa taka zinazotokana na huduma za afya pamoja na kuweka miundombinu sahihi ya kuteketeza taka (incinerator).
Agizo hilo limetolewa tarehe 16.05.2024 na Kaimu Mkurugenzi Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria Bw. Hamad Taimuru Kissiwa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa NEMC Dar es salaam kufuatia tatizo la utupaji holela wa taka zitokanazo na huduma za afya katika maeneo mbalimbali yasiyokua rasmi.
Bw.Taimuru amesema kumekuwa na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka zitokanazo na huduma za afya hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira na kupelekea athari kwa binadanu na viumbe wengine ikiwa ni pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza na magonjwa ya mlipuko.
Amesema taka nyingi ni zile zenye ncha kali, viungo vya mwili, material za vitambaa, damu mgando zinazotupwa bila utaratibu baada ya huduma hali inayohatarisha afya ya jamii na mazingira.
Bw. Taimuru amezielekeza Mamlaka za udhibiti nchini zinazoshughulikia usimamizi wa taka hatarishi zinazotokana na huduma za afya kuhakikisha wanafuata Miongozo iliyowekwa na Wizara pamoja na masharti ya Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa taka hatarishi
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15