​NEMC YASHIRIKI UFUNGUZI WA MAONESHO YA 48 YA KIMATAIFA YA BIASHARA.


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki ufunguzi wa maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara yaliyohusisha Nchi 26 na washiriki 3846 yaliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.

Ufunguzi huo umefanywa na Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Jucinto Nyusi akiambatana na mwenyeji wake Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.

Katika ufunguzi huo pia umehudhuriwa na washiriki kutoka Taasisi za umma na binafsi, makampuni binafsi,ofisi za Serikali, wizara, vyuo vikuu, wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara