NEMC yajipanga kutoa Elimu kwa Wamiliki wa Baa na Kumbi za Starehe nchi nzima
NEMC YAJIPANGA KUTOA ELIMU KWA WAMILIKI WA BAA NA KUMBI ZA STAREHE NCHI NZIMA
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr. Samuel G. Mafwenga amewataka wamiliki wa Baa na Kumbi za starehe kuendesha shughuli zao bila kufanya uchafuzi wa kelele kwa wananchi wanaokaa karibu na shughuli hizo, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Nchini, wamiliki wa Baa na kumbi za starehe wajijini Dar es Salaam katika ukumbi wa LAPF Millenium Tower.
Alisema kuwa “Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira limekuwa likipokea malalamiko mengikutoka kwa wananchi kuhusu kero na usumbufu mkubwa wanaopata kutokana na kelele kutoka kwa baadhi yenu mnaoendesha shughuli hizo”
Kutokana na kelele hizo zinazolalamikiwa Baraza limejipanga kutoa elimu kwa wadau wote wanaomiliki vyombo hivyo vya starehe ili kuwapa elimu juu ya namna ya kudhibiti kelele hizo ili zisiwe kero kwa wengine. Kulingana na shughuli hizi kufanyika katika makazi ya watu baraza halinabudi kuandaa mikutano mbalimbali nchini kuwaelimsha wamiliki kutumia chombo cha udhibiti wa kelele kuepuka malalamiko yanayotolewa na wakazi wa maeneo husika. Kutokana na hayo, Baraza limeanza kutoa elimu kwa wamiliki wa baa na kumbi za starehe kwa mkoa wa Dar es Salaam na kufuatiwa na Mkoa wa Pwani. Bugudha inayotokana nakelele, mbali na tafiti na chambuzi mbalimbali imethibitisha kuwa kelele hizo zina athari kubwa kwa wananchi ikiwemokukosa usingizi, wazee na wamama wajawazitokukosa kupumzika vizuri wakati wa mchana na usiku, presha, ukiziwi hata hivyo zinaathari kubwa kwa wanaume zinapelekea kupungua kwa nguvu za kiume.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Benard Kongola alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wadau na kutoa vifungu vya Sheria na Kanunizinazodhibiti kelele na mitetemo.alisema kuwa kwa mujibu wa sheria kelele ni sauti isiyokubalika na inayoudhi ambayo inamadhara au inaweza kuwa na madhara kwa afya ya Binadamu na Mazingira. Aidha, alitoa kifungu cha Sheria ambacho kilitangazwa katika gazeti la serikali (GN) Namba 32 la tarehe 30 January, 2015. Kanuni hizi zilitungwa kwa mujibu wa kifungu namba 230 (2) (s) cha sheria ya Usimamizi wa Mazingiraya Mwaka, 2004.
Hata hivyo Dr. Gwamaka alimalizia kwa kusema kuwa kutokana na sheria na kanuni za udhibiti wa kelele, NEMC ikiwa ni Taasisi ya serikali inahaki na wajibu wa kutekeleza sheria hiyo, hivyo kwa sasa wamejikita katika kutoa elimu zaidi na baadaye hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakao kaidi agizo hilo.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15