NEMC YAENDESHA ZOEZI LA UTEKETEZAJI DAWA ZILIZOKWISHA MUDA WAKE -KILIMANJARO


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini, Manispaa ya Moshi na Jeshi la Polisi Wilaya ya Moshi wasimamia zoezi la uteketezaji wa dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi na vifaa tiba kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini- Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC)

Zoezi hilo limefanyika kwa kutumia incinerator la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba kwa ustawi wa afya zetu na mazingira kwa ujumla