โNEMC KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KUJIRIDHISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA KWA MUJIBU WA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza utaratibu wa kupitia miradi yote iliyopatiwa vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) ili kujiridhisha kama wamiliki wa miradi hiyo wanatekeleza matakwa ya kisheria yaliyoainishwa kwenye vyeti hivyo wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria NEMC Bw. Hamadi Taimuru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwenendo wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria katika eneo la Tathmini ya Athari kwa Mazingira.
Bw. Taimuru amesema Baraza limefikia uamuzi huo baada ya kuona miradi mingi haifuati masharti yaliyoainishwa kwenye vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira kuhakikisha kwamba Mazingira yanaendelea kutunzwa wakati wa utekelezaji wa mradi na baada ya kukamilika kwa mradi.
โTumeandaa mkakati wa kuwafuata mmoja mmoja kukagua na kujiridhisha matakwa ya cheti na wao wanafanya nini kwa lengo la kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa safi na salama na wananchi wakae katika mazingira yenye afya na hata kazi zao ziweze kwenda vizuriโ Amesema Bw. Taimuru.
Akizungumzia kuhusu kaguzi za kila mwaka za mazingira Bw. Taimuru amesisitiza wawekezaji kujikagua na kuwasilisha taarifa zao Baraza ili zipitiwe na kujiridhisha huku akiwashukuru wawekezaji waliokwisha kufanya hivyo na tayari taarifa zao zimeshapitiwa na Baraza na kujibiwa kwa mujibu wa Sheria.
Naye Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Irene John amesisitiza kuwa Baraza litaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kufanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira kabla ya kuanza miradi ili Tanzania iendelee kuwa salama kwa wageni, wenyeji , wanyama na hata vizazi vijavyo kwamaendeleo endelevu ya Taifa letu
๐๐ฌ๐ข๐ฌ๐ข๐ญ๐ข๐ณ๐ ๐๐ก๐ข๐๐๐๐ก๐ข ๐ง๐ ๐๐ฌ๐ข๐ฆ๐๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ณ๐ข๐ง๐ ๐ข๐ซ๐ ๐ก๐๐ฌ๐ ๐ฎ๐๐ก๐ข๐๐ข๐ญ๐ข ๐ฐ๐ ๐ค๐๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐๐ก๐๐๐ฎ๐ณ๐ข...
Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingir...
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15

