ELIMU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA YATOLEWA BANDA LA NEMC MAONESHO YA MBEYA CITY EXPO 2024
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limejipanga kutoa elimu kwenye maeneo sita ikiwamo utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wananchi, wawekezaji, wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zilizopo Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza jana na wananchi kwenye Maonesho ya Mbeya City Expo 2024, Meneja wa Kanda hiyo, Josiah Murunya, alisema NEMC inashiriki Maonesho hayo na itatoa Elimu kwenye maeneo sita ambayo hatua za kuzingatia wakati wa kufanya Tathimini ya athari kwa Mazingira (TAM), katazo la mifuko ya plastiki, namna ya kusajili miradi NEMC kwa kutumia mfumo kielekitoniki (PMS).
Alisema pia eneo jingine wanalotoa elimu ni uchafuzi wa mazingira yatokanayo na kelele na kusikiliza kero na kutatua malalamiko yanayotufikia yanayohusu uchafuzi wa mazingira.
"Kauli mbinu ni kuchochea uwekezaji na biashara kwa uchumi endelevu, tutatumia maonesho haya kuitangaza NEMC na majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa wananchi, wawekezaji na wafanyabiashara wanaoshiriki na kuhudhulia maonyesho hayo,"alisema.
Alitoa wito kwa wawekezaji waliyopo kwenye maonesho na wafanyabiashara wapate elimu ya kufanya Tathmini ya Mazingira katika miradi yao.
"Tunajenga na kuendeleza mahusiano kati ya Baraza na Wananchi, wawekezaji, wafanyabiashara , Taasisi za Serikali na Binafsi, kujifunza mambo mapya yatakayosaidia kuboresha utoaji wa huduma zetu,"alisema.
Alibainisha kuwa kumekuwapo na uelewa mdogo wa wanachi na wafanya biashara kuhusu sheria ya Mazingira na Kanuni zake, hivyo kupitia maonesho hayo Baraza litaweza kutangaza huduma linazotoa kwa wananchi na wadau mbalimbali wa Mazingira.
"Tunatarajia wawekezaji na wafanyabiashara wengi waliyo na miradi wataweza kusajili miradi yao katika Baraza, Wawekezaji na wananchi watajua wajibu wao katika kutunza na kuhifadhi Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake ikiwa ni pamoja na kulipa Ada na Tozo za Mazingira kwa miradi inayofanya kazi,"alisema
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15