NEMC NA TIMU YA UFUATILIAJI MIRADI KUTOKA MFUKO WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI YATUA MANYONI
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Timu ya ufuatiliaji miradi (Project Monitoring Mission) kutoka mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi (Adaptation Fund) watembelea Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni juu ya mradi wa uvunaji maji kimkakati (SWAHAT) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA).
Wakati wa mazungumzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota amelishukuru Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kuleta mradi katika Wilaya yake na kusisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika kutekeleza mradi huo ili uweze kuleta tija iliyokusudiwa
Naye Bi. Anastazia Tutuba Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Manyoni alipopata wasaa wa kuzungumza aliushukuru ufadhili wa mfuko huo na kuahidi kuendelea na Mradi katika usimamizi mara utakapo kabidhiwa kwenye Halmashuri yake.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15