NEMC KUWACHUKULIA HATUA WALE WASIOZINGATIA SHERIA ZA VIWANGO VYA KELELE


Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, limewakumbusha viongozi wa nyumba za ibada na sehemu za starehe kuzingatia sheria za viwango vya kelele la siyo watavifungia mara moja kwa kukiuka sheria hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa NEMC,Dkt Samweli Gwamaka, amesema kuwa hivi karibuni wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu mbalimbali juu ya ukiukaji wa sheria ya kiwango cha kelele kutoka kwenye bar na nyumba za ibada hali ambayo inaleta kero kwa wananchi.

Amesema kuwa wamekuwa wakitoa viwango vya upigaji wa kelele kwa muda wa usiku na mchana hivyo kwa atakayekiuka agizo hilo watakaokiuka watawafungia au kuwachukulia vifaa vyao ikiwemo kuwapeleka Mahakamani kwa kosa la uvunja sheria ya viwango vya kelele

Aidha Dkt,Gwamaka amesema kuwa ni vema wahusika wa shehemu za starehe na nyumba za ibada kuweka mfumo wa kuzuia sauti kutoka nje (Sound prof) na kuweza puguza bugudha kwa watu wengine. Amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wahusika juu ya kuzingatia sheria ya viwango vya kelele na kuzingatia kutokujenga nyumba ya ibada na shehemu za starehe karibu na makazi ya watu ikiwa ni hivyo basi kuzingatia kutokupiga kelele.

Dkt, Gwamaka ameongeza kuwa kwa kipindi hiki wanakesi Tatu na ziko mahakamani kwa uvunjifu wa sheria hiyo na bado wanaendelea kufanya msako kwa watu watakaokiuka sheria hiyo. Katika hatua nyingine amesema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa viongozi pwa nchi na wadau mbalimbali ya uvunjifu wa sheria hiyo hivyo kuonekana kuwa kero kubwa kwa jamii

AmewatakaWananchikutoa ushirikiano kwa NEMC kwa kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za upigaji wa kelele ili kuweza kudhibiti tatizo hilo linalojitokeza kwa jamii kwa hivi karibuni.