NEMC KANDA YA MOROGORO RUFIJI YATEMBELEA GHALA LA KUTENGENEZA MKAA MWEUPE


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Morogoro Rufiji yatembelea ghala la Kampuni ya Viridium Tanzania Limited inayojishughulisha na utengenezaji wa nishati mbadala ya kupikia maarufu kama mkaa mweupe.

Kampuni hii kiwanda chake kipo Iringa na Morogoro. Inatengeneza mkaa huo mweupe kutoka kwenye nyasi ziitwazo "Elephant grasses" kwa kutumia mashine maalum.

Ofisi ya Kanda pia imetembelea shule ya awali na shule ya msingi ya Wesley pamoja na Mama lishe ambao ni watumiaji wa mkaa mweupe huo. Watumiaji hao wamekiri kuwa mkaa mweupe ni mzuri kwa kupikia, unaokoa gharama na unalinda mazingira.