​NEMC IPO KAZINI VIWANJA VYA SABASABA


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendelea kutoa elimu ya Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira kwa wananchi.

Elimu hiyo imehusisha umuhimu wa ulipaji wa Ada za Mazingira, usimamizi wa taka hatarishi na athari zake, matumizi salama ya Kemikali ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa dhahabu pamoja na umuhimu wa kutenganisha taka kutoka kwenye chanzo.

Tunaendelea kuwakaribisha wananchi katika Banda letu lililopo viwanja vya sabasaba jengo la Karume ili kupata elimu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa