MFUKO WA DUNIA WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI (ADAPTATION FUND) UMEPITISHA MIRADI MIWILI ITAKAYO RATIBIWA NA NEMC YENYE THAMANI YA KIASI CHA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 2.2
Mfuko wa dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi (Adaptation Fund) kupitia kwa Bodi ya taasisi hiyo (Adaptation Fund Board) umepitisha miradi miwili kati ya minne iliyowasilishwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 2.2.
Miradi hiyo ambayo ni, โKukabili Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Jamii ya Wafugaji na Wakulima Wilaya ya Kongwa na โโKukabili Mabadiliko ya Tabia ya nchi katika jamii za Pwani ya Zanzibarโ yote ikiwa na lengo la kutatua changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo hayo.
Miradi hii miwili nchini itaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamamizi Wa Mazingira (NEMC) na kutekelezwa na taasisi zilizoshinda miradi hiyo (Excuting Entities) ambazo kwa mradi wa Kongwa ni Foundation For Energy, Climate and Environment (FECE) inayoshirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na mradi wa Zanzibar ni Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Baraza linasubiri majibu ya miradi miwili iliyobaki kati ya minne iliyowasilishwa kwa taasisi hiyo.
Aidha kupitishwa kwa miradi hiyo ni mafanikio makubwa kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na kuwa mratibu wa mfuko huo hapa nchini.
๐๐ฌ๐ข๐ฌ๐ข๐ญ๐ข๐ณ๐ ๐๐ก๐ข๐๐๐๐ก๐ข ๐ง๐ ๐๐ฌ๐ข๐ฆ๐๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ณ๐ข๐ง๐ ๐ข๐ซ๐ ๐ก๐๐ฌ๐ ๐ฎ๐๐ก๐ข๐๐ข๐ญ๐ข ๐ฐ๐ ๐ค๐๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐๐ก๐๐๐ฎ๐ณ๐ข...
Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingir...
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15

