MKURUGENZI MKUU WA NEMC ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KILIMANJARO KUTATHMINI ATHARI YA MOTO.


Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alitembelea Hifadhi ya Taifa yaKilimanjaro ku tathmini uharibifu uliojitokeza baada ya kutokea mlipuko wa moto katika hifadhi hiyo akiambatana na Meneja wa NEMCKanda ya Kaskazini Bw. Lewis Nzali na wataalamu wengine wa mazingira kutoka NEMC, ambao ni Bw. Fredrick Mulinda naBi. Nancy Nyenga. Dkt Gwamaka alisema jambo kubwa la kushukuru hapakutokea maafa makubwa kwa uhai wa wanadamu naMazingira ni lazima yatunzwe kwa gharama yoyote kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo hivyo alishauri uwekwe utaratibu mzuri wa tahadhari za kujikinga na moto pamoja na kuhakikisha majani yasiwe karibu na kambi zote.

“Tunamshukuru Mungu hakuna maafa makubwa lakini ni wajibu wetukuhakikisha mazingira yanatunzwa ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo mizuri ya kudhibiti majanga kama ya moto yasilete madhara makubwa katika mazingira hii itasaidia kulinda uhai wa viumbe vilivyopo kwenye hifadhi kama wanyama, mimea, wadudu wasiathirike. Tukiwa tayari na mipango mikakati kabla ya dharura kama hizi itasaidia pia kuweka mazingira mazuri katika mfumo wa ikolojia. Nashauri katika kambi zote uwekwe utaratibu ambao majani yasiwe karibu na eneo la kambi ili kunusuru hali hii isijitokeze tena.

Nao Wataalamu wa Mazingira kutoka NEMCwaliwashauri wasimamizi wa Hifadhi hiyo kuboresha Mpango wa Usimamizi ili ujumuishe mbinu bora za kuzuia na kudhubiti moto na pia wawekeze kwenye mbinu za kisasa za kupambana na moto kama vile kutumia helikopta pamoja na kuweka ukanda wa kutenganisha eneo la watalii na misitu.