​MAAFISA FORODHA MPAKA WA TUNDUMA NA MAAFISA MAZINGIRA WA MIKOA YA SONGWE NA MBEYA WAPATIWA MIONGOZO NA ELIMU YA MATUMIZI SALAMA YA ZEBAKI


Maafisa Forodha wa mpaka wa Tunduma na Maafisa Mazingira wa Mikoa ya Mbeya na Songwe wapatiwa mafunzo juu ya Muungozo wa Uingizaji na Utumiaji wa kemikali ya Zebaki nchini.

Mafunzo hayo yametolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika ofisi za mpaka wa Tunduma Mkoa wa Songwe.

Akitoa mafunzo hayo Bw. Boniface Kyaruzi Mhandisi Mazingira wa NEMC amesema ni kwa lengo la kuwajengea uelewa wa namna sahihi ya usimamizi, uingizaji halali na matumizi salama ya kemikali ya zebaki kwa wachimbaji wadogo ili kuepuka athari za kiafya na kimazingira

Bwana Kyaruzi ameongeza kuwa mafunzo haya yanayoendeshwa kupitia Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Kemikali ya Zebaki (EHPMP) unaofadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni mahususi kwa ajili ya utekelezaji wa maazimio ya Mkataba wa MINAMATA wenye takwa la kuandaa mpango kazi wa Kitaifa kwa kil Nchi mwanachma wa namna sahihi ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo kwa dhumuni la kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya madhara yanayotokana na uchafuzi unaotokana na zebaki.

Naye Bw. Jansen Bilaro Mkemia kutoka Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mbeya alipozungumza amewataka Maafisa hao kushirikiana bega kwa bega na Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kudhibiti uingizaji haramu na matumizi yasiyo salama ya kemikali ya zebaki kwa kuhakikisha waingizaji, wasambazaji na wachimbaji wadogo wanasjiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali Na.3 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ikiwemo zebaki