JAFO ASHIRIKI KUFANYA USAFI , KUPANDA MITI KIGAMBONI NA KISARAWE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Seleman Jafo ameshiriki katika zoezi la kusafisha maeneo ya fukwe wilaya ya Kigamboni mapema Leoasubuhiikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa kampeni ya SOMA NA MTI ambayo tayari ilishazinduliwa katika wilaya za Ubungo na Temeke mkoa wa Dar es salaam.

Waziri Dkt. Jafo amesema adhima ya serikali ni kutaka kuona maeneo yote wanayokaa watu ikiwemo maeneo ya stendi za mabasi, daladala, masoko, maeneo ya biashara mbalimbali, taasisi za Serikali zote zinatakiwa kuwa safi. "Ndio maana nimeona piga uwa garagaza ni lazima Leo niwe na wakazi wa Kigamboni katika agenda hii ya usafi na kupanda miti Kwa sababu ninyi mnatekeleza maagizo ya serikali Kwa asilimia miamoja".

Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi Kwa Sasa yamebadilika sana ndio maana ni lazima tupande mitina tutunze mazingira ndio maana tumekuwa na kampeniya SOMA NA MTI lengo letu ikiwa ni kupanda miti million mia mbili na sabini na sita(276,000,000) Kwa mwaka, Kila Halmashauri ipande miti millionMojana nusu(1,500,000)."Kampeni ya SOMA NA MTI inamtaka Kila mwanafunzinchini Tanzania apande Mti na tuna wanafunzi milioni kumi na nne na nusu(14,500,00) wale wa Shule za msingi, Sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu".

Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi na kupanda miti katika wilaya ya Kigamboni waziri Jafo alielekea katika kongamano la kutunza na kuhifadhi mazingira lililoandaliwa na wadau wa mazingira wa taasisis isiyokuwa ya kiserikali ya World WideLife Fund(WWF) ikishirikiana na Vodacom Foundation Tanzanian iliyofanyika katika Msitu wa Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, ambapo pia kulikuwa na zoezi la upandaji Mitina kuzindua utumiaji wa jiko banifu ambalo ni rafik sana Kwa kuhifadhi mazingira.

"Leo nimefarijika sana wadau wetu wa WWF mmeungana na Vodacom Foundation Tanzanian na wadau wengine wote Kwa kuhakikisha tunaendesha zoezi kubwa la upandaji Miti Kwa ajili ya kunifanya Tanzania kuwa ya kijani zoezi ambalo linafanyika ndani ya Msitu maarufu nchi kwetuKazimzumbwi, sambamba na hilo nifarijike sana Leo kazi hii ikiendelea inaenda sambamba na swala Zima la utunzaji mazingira kwanza upandaji Miti lakin kusaidia juhudi mbalimbali za kufanya tunatumia miundombinu iliyosahihi Kwa ajili ya kupunguza uharibifu wa mazingira nimefurahi sana Kwa kunikaribisha katika ugawaji wa jiko hili banifu linalopunguza utumiaji wa Kuni kutoka Kuni elfu tatu(3,000) mpka Kuni mia nne (400)".

.