​ELIMU YA MADHARA YA ZEBAKI YATUA KWA MAAFISA FORODHA MPAKA WA TUNDUMA NA MAAFISA MAZINGIRA MIKOA YA SONGWE NA MBEYA .


Elimu ya madhara ya zebaki kupitia mradi wa kidhibiti matumizi ya kemikali ya zebaki unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na ofisi ya maabara ya mkemia Mkuu wa Serikali yatolewa kwa Maafisa forodha mpaka wa Tunduma na Maafisa Mazingira Mikoa ya Songwe na Mbeya

Akitoa elimu hiyoBi. Zabibu Nduru Mkemia Mwandamizikutoka Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dodomaamesema amesema zebaki iko katika hali ya kimiminika kizito na ni moja kati ya vyanzo kumi vinavyohatarisha zaidi afya ya jamii kutokana nashughuli za kibinadamu.

Amesema matumizi yasiyo salama ya kemikali ya zebaki huleta athari za kiafya na kiamzingira ikiwa ni pamoja nakuharibu figo, ini na mapafu, kuharibu mfumo wa fahamu na viungo muhimu vya mwili hali inayopelekeakushindwa kuhisi, kukakamaa kwa mwili, macho kuharibika, kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa ngozi, kupoteza nguvu za kiume, msongo wa mawazo, kuwashwa kwa ngozi na mwili kudhoofika.

Bi.Zabibu Nduru ameongeza kuwa kwa mama wajawazito huathiri ukuaji wa mtoto kwa sumu kupita kwenye kondo la mama, kupoteza nguvu za kiume kwa wanaume, msongo wa mawazo na mwili kuwasha na kupungua.

Ameyafafanuamadhara ya zebaki yanayotokeaikiwa mtu hatavaa vifaa kingawakati wa kuchenjua madini na wakati wa kuchoma zebaki iliyokamata madini ili kuiachanisha, hivyo nivema wachimbaji wakatumia vifaa Kinga ili kujilinda dhidi ya athari za zebaki.

Naye Bi.Joyce Njisya Meneja Usajili wa Maabara kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dodoma, amewataka wasimamizi na watendaji wa mpaka wa tunduma kushirikianakwa karibu kuthibiti madhara yatokanayo na matumizi ya zebaki,na kuhakikisha wanasimamia ipasavyousafirishaji halali wa zebaki na matumizi salama ili kuepuka uingizaji wa zebaki kinyemela na iliyo chini ya kiwango na kuepuka madhara ya zebaki

Aidha ametoa Wito kwa wafanyakazi wa maeneo yote yanayotumia zebaki kuhakikisha wanatumia zebaki iliyo sajiliwa na Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali na atakae kamatwa na zebaki kinyume na umiliki uliodhinishwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

"Nchi yetu bado inaruhusu matumizi ya zebaki, rai yangu kwa makampuni na watu binafsiwanaojihusisha na usafirishaji usamabazji na utumiaji wa kemikali ya zebaki, kuhakikisha wanasajiliwa na kupewa vibalikwa mujibu wa sheria, ikibainika kukiuka sheriai faini ni kuanzia million moja hadi 200 huku mtu binafsi faini yake ni kuanzia laki moja hadi million 2.5" ameeleza Bi.Joyce Njisya.

AfisaForodha wa mpaka wa Tunduma Bwa.Menlad Mpangala kwa niaba ya washirikiwote wa mafunzo ameishukuru NEMCna GCLAkwa kutoa elimu ya matumizi salama ya zebaki kwani kupitia elimuhiyo itawasadia kudhibiti usalama wa kusafirishazebaki katika mpaka wa Tunduma one stop bounder post.

Ameongoze kwa kusema wasafirishaji wa zebaki waache kupitisha zebaki kiholela kwanikufanya hivyo kunapelekea kuingiza nchini kemikali ya zebaki isiyokua na kiwango, watanzania kutumia kemikali hiyo kwa kificho na kuwasababishia madhara nakuikosesha Serikali mapato