DAR ES SALAAM BILA KELELE CHAFUZI ZA MAZINGIRA NA MIFUKO YA PLASTIKI INAWEZEKANA - RC MAKALA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalaamewataka wananchi pamojana wamiliki wa kumbi za burudani na viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kuhakikisha wanazingatia misingiya Sheria na weledi katika kutekeleza majukumu yao kwa mustakabali mpana wa Mazingira na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa leo katika mkutano wa pamoja na wadau wa mazingira kwa lengo lakujadili suala la udhibiti wa viwango vya kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliofanyikakatika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Makala amesema Dar es salaam imekuwa nachangamoto kubwa ya viwango vya juu vya kelele katika kumbi za burudani Hali inayoleta bugudha kwa wakazi na kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki inayoharibu ikolojia ya wanyama na uoto wa asili.

Amesema "Dar es salaam bila mifuko ya plastiki na kelele zilizokidhi viwango inawezekana na ni wakati wa kila mmoja kuwajibika na kuhakikisha haki inatendeka bila kupepesa macho na kwa wazalishaji kusalimisha mifuko ya plastiki waliyoizalisha katika ofisi za NEMC bila kuchukuliwa hatua."

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amewataka wananchi kufuata Kanuni na Sheria za Uhifadhi wa Mazingira kwa kudhibiti viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali hususani kumbi za starehena kuwasisitiza kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kwani ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira.

Amesisitiza kuwa "wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mifuko ya plastiki wahakikisheviwanda vyao vinasajiliwa na Baraza na kupatacheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kabla ya kuanza uzalishaji na kufuata matakwa ya Sheria na viwango sahihi vilivyowekwa."

Kadhalikaametoa angalizokwa wazalishaji nawasambazaji wa mifuko ya plastiki kujisalimisha kwani Baraza litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa juu ya uwepo wa kiwanda au wasambazaji wa mifuko na vifungashio visivyokidhi viwango.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt. Athuman Ngenya amesema "wale wote wanaomiliki viwanda vya kuzalisha plastiki ambao wana leseni ya TBS endapo watahitaji kuhuisha leseni au kuchukua leseni mpya lazima wawe na Cheti cha Mazingira kutoka NEMC.

Katika hatua nyingine Mhe.Makala ametoa muda wa wiki moja kwa NEMC na TBS kuandaa ratiba ya kuzunguka kwenye m

Mitaa na Kata katika kutoa elimu ya Mazingira.