BODI YA WAKURUGENZI YA NEMC YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM


BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepanga kukutana na waagizaji wa mafuta nje ya nchi na wanaopokea mafuta hayo kwenye matenki bandarini kujadili ni jinsi gani wanaweza kuboresha miundombinu ambayo imekuwa sehemu ya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari.

Ameyasema hayo jana Februari 23,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka wakati Bodi na Menejimenti ya Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutembelea katika eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hay

Akizungumza na Waaandishi wa habari Dkt.Gwamaka amaesema kuna changamoto ambazo wamezipokea kutoka uongozi wa bandari, katika changamoto hizo sehemu kubwa ni changamoto zinazohusiana na upokeaji wa mafuta ikiwa ni pamoja na mambo yanayopokea mafuta kuchakaa kutokana na kutumika kwa muda mrefu zaidi ambayo yanamilikiwa na watu binafsi.

“Mara nyingi tumekuwa tukiwasiliana na wawekezaji wengi katika eneo hili ambapo unakuta mafuta yanatapakaa baharini kwasababu kubwa ni ubovu wa miundombinu ya mabomba ya kupokea mafuta kwenye meli hivyo tukikaa nao tutazungumza kuona ni namna gani wanaweza kuboresha miundombinu hii kusiweze kuleta athari zozote za kimazingira”. Amesema Dkt.Gwamaka

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Mrisho Mrisho amesema wamekuwa wakifanya shughuli zao bila uchafuzi wa kimazingira, hivyo wamepokea ushauri kutoka NEMC hasa kwenye masuala mazima ya miradi , kuhakkikisha wanaangalia sula zima la utuzunzaji wamazingira.

“Wakati wote wa ufanyaji wa hii miradi tumefanya kazi na NEMC kwa ukaribu na kila wakati tunawafuata na kuwaambia kile tunachoendela nacho

Pamoja na hayo amewapongeza NEMC kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye kuhakikisha miradi ambayo inatekelezwa na bandari inaenda sambamba na kuhakikisha utunzaji wa mazingira hivyo wapo tayari kuendelea kupokea ushauri wowote wanaopewa wenye lengo la kuhifadhi mazingira.

Nae Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofiisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema miradi mingi ambayo wameiona kwenye bandari hiyo kwa namna moja ama nyingine ina muingiliano mkubwa na sekta zingine hivyo wanashauri Mamlaka ya Bandari ikafanye Tathiminni ya Kimkakati ya Mazingira ili sekta zote zinazoonekana zinashabiana na shughuli zinazoendelea bandarini ziweze kushirikishwa ili tuone kwa namna gani kwa pamoja tunaweza kwenda mbele.