ππππ ππ πππ πππππππππ ππππππ ππ ππππππππππ πππππ π ππ ππππππ ππππππππ ππ ππππππ ππ πππππππππππ ππ ππππ πππππ
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kwa kushirikiana na kituo cha sayansi na Mazingira India CSE limeendesha warsha iliyolenga kujengeana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja juu ya mifumo endelevu ya usimamizi na udhibiti wa taka ngumu. Warsha iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye Warsha hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema ushirikiano wa Baraza na CSE unalenga kuboresha mbinu za kusimamia Mazingira hasa kujengeana uzoefu na kutoa elimu kwa wananchi na wadau juu ya umuhimu wa urejelezaji wa taka ngumu.
βNEMC pamoja na CSE tunasimamia Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira, moja ya maeneo tunayofanyia kazi ni usimamizi wa rasilimali taka ambazo zinaonekana kama uchafu lakini kwetu sisi ni fursa. Hivyo tunataka kuainisha mchakato mahususi kwa kushirikiana na Halmashauri zote kupitia TAMISEMI ili kuboresha mifumo ya usimamizi wa taka ngumu pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kurejeleza taka ngumu ili wananchi wajipatie kipato na kutunza Mazingira kwa wakati mmojaβ amesema Dkt. Immaculate Semesi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwandamizi wa CSE Bw. Aditya Batra amesema ushirikiano na NEMC umewaleta karibu na wadau mbalimbali kama Halmashauri za Jiji na Manispaa pamoja na TAMISEMI ambao ndio walengwa wa kusimamia taka ngumu na kutoa elimu kwa wananchi juu ya urejelezaji wa taka ngumu.
Naye Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira NEMC Dkt. Menan Jangu ameongeza kuwa NEMC itaendelea kushirikiana na wadau ili kupata mbinu au mifumo sahihi ya kiteknolojia ya urejelezaji wa taka ngumu.
Kadhalika, Mratibu wa Huduma za Afya na Usafi wa Mazingira TAMISEMI Bw. Selemani Yondu amesema wanafurahi kupata uzoefu zaidi kutoka NEMC na CSE ili kudhibiti taka ngumu na kutunza Mazingira.
Warsha hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sayansi na Mazingira India CSE kwa kushirikiana na NEMC, washiriki wengine ni TAMISEMI, Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam na asasi za kiraia zinazohusika na taka ngumu.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15