NEMC YAWATAKA WAWEKEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KUFANYA KAGUZI BINAFSI KUEPUKA ATHARI KWA JAMII NA MAZINGIRA
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lawataka wenye miradi ya maendeleo kufanya kaguzi binafsi kila mwaka baada ya kupata cheti cha mazingira ili kujitathmini mwenendo wa uendeshaji mradi na utekelezaji wa masharti ya Cheti cha Mazingira.
Hayo yamesemwa na Meneja wa NEMC - Kanda ya Temeke Bw. Arnold Mapinduzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zinazofuata baada ya mwenye mradi wa maendeleo kupata cheti cha Mazingira ambapo moja ya masharti ni kufanya ukaguzi binafsi kila mwaka na kuwasilisha taarifa kwa Baraza. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Arnold Mapinduzi amesema; baada ya mwenye mradi wa maendeleo kupata cheti cha mazingira, Sheria inamtaka kufanya ukaguzi binafsi kila mwaka na kuwasilisha taarifa hizo kwa Baraza ili kufanya Tathmini ya uendeshaji wa mradi na utekelezaji wa masharti aliyopewa yenye dhumuni la kulinda na kutunza Mazingira.
“Baada ya mwekezaji kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na kupata cheti cha Mazingira, Sheria inamtaka kufanya ukaguzi binafsi wa mradi wake kila mwaka na kuwasilisha taarifa hiyo Baraza. Lengo kujitathmini mwenyewe katika uendeshaji wa mradi wake, kuhakikisha kuwa utekelezaji wa masharti ya cheti cha Mazingira kuwasilisha taarifa hiyo ili Baraza kuona kama kuna changamoto liweze kumsaidia kwa Ushauri” amesema Bw. Mapinduzi.
Akizungumzia kuhusu kaguzi binafsi za Mazingira za kila mwaka, Bw. Mapinduzi amesisitiza wenye miradi kujikagua na kuwasilisha taarifa sahihi kwa Baraza ili zipitiwe na kutoa ushauri sawia utakaowezesha kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa wawekezaji wenyewe na kwa jamii.
Naye Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Irene John alipozungumza amesisitiza kuwa Baraza litaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kaguzi binafsi za Mazingira baada ya kuanza kwa mradi ili kulinda viumbe hai na Mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo na hivyo kuwezesha maendeleo endelevu ya jamii na Taifa letu kwa ujumla
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15