HALMASHAURI ZILIZOPO UKANDA WA PWANI ZIPANDE MITI YA MIKOKO- WAZIRI JAFO.
HALMASHAURI ZILIZOPO UKANDA WA PWANI ZIPANDE MITI YA MIKOKO- WAZIRI JAFO.
Halmashauri zilizopo ukanda wa pwani hasa katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Tanga, Pwani na Dar es salaam zimetakiwa kupanda miti ya mikoko katika maeneo ya pembezoni mwa bahari ili kutunza mazingira. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo lekatika zoezi la upandaji miti ya mikoko liliofanyika katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
“Upandaji miti ya mikoko ukanda wa Pwani ni muendelezo wa maelekezo ya Serikali katika ukanda huu kwani miti hii inafaida kubwa katika mazingira katika kupambana na hewa ukaa”
Hata hivyo waziri Jafo amewataka wanachi kulinda mazingira ili kukabiliana na ukame huku akiwaonya wanaokata miti ya asili kwa ajili ya mkaa , wanao chepusha mito na kuvunja kingo za mito kuacha mara moja , aidha Jafo amewaomba Wakala wa Misitu Tanzania TFS kusimamia upandaji miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
Aidha waziri Jafo ameipongeza wilaya ya Bagamoyo kwa kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Raisi naWaziri Mkuu katika zoezi la upandaji miti, pia Mhe. Jafo ameyaomba maeneomengine kuendeleza zoezi la upandaji miti ya mikoko kwa kuitunza na kuilinda.
Naye katibu tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni amemshukuru waziri Jafo kwa uzinduzi huo wa upandaji miti ya mikoko katika wilaya yao,Bi. Mgeni amesema kuwa wilayahiyo imekuwa ikiendeleza zoezi la upandaji miti kwani imefanikiwa kupanda miti laki nane themanini elfu(880,000) kwa mwaka wafedha 2021/2022 na mwaka2021/20 22 laki sita sitini na nane efu (660,000), ili kutekeleza maelekezo ya selikali ya upandaji miti milioni 1.5 kwa kila wilaya.
Pia waziri Jafo amewasihi wa Tanzania wote kupanda miti kipindi hiki cha Mvua na kuwataka walimu kusimamia wanafunzi katika ajenda ya upandaji miti ilikutekeleza ajenda ya serikali ya kupanda miti Milioni 276 kila mwaka kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa Halmashauri 184, ili kulinda mazingira yetu.
-
Maazimisho
2020-01-21
-
Kongamano la Kisayansi
2023-08-28
-
Wiki ya Utumishi wa Umma
2019-12-15